Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana awataka viongozi wa Serikali kurahisisha shughuli za wananchi

K4 Kinana awataka viongozi wa Serikali kurahisisha shughuli za wananchi

Tue, 26 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg. Abdulrahman Omar Kinana amewataka viongozi na watendaji wa serikali kuhakikisha wanarahisisha ufanyaji wa shughuli za wananchi kwa kuwaondolea vikwazo kwa kuwa sekta binafsi inaanza na wao.

Kinana ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini eneo la Lyazumbi wakati wa mapokezi ya kuanza ziara mkoani Rukwa akitokea mkoa wa Katavi.

“Serikali inafanya jitihada za kuimarisha na kuboresha mazingira ya sekta binafsi nchini ili ifanye vizuri, sasa sekta binafsi inaanza na wananchi wa kawaida. Tuwaondolee kero wananchi wetu na tuwarahisishie kufanya shughuli zao iwe ni wakulima, wafugaji, bodaboda, wamachinga au wafanyabishara.” Amesema Kinana

Akimkaribisha mkoani Rukwa Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Ndugu Rainer Lukalah amemueleza Ndg Kinana kuwa hali ya siasa katika mkoa huo ni shwari na wanaridhishwa na kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kinana ameingia mkoani Rukwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya uimarishaji chama na ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live