Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana ataja dhamira ya Rais Samia uchaguzi 2025

Spika Tulia, Kinana Watoa Ya Moyoni Bwawa La Mwalimu Nyerere.jpeg Kinana ataja dhamira ya Rais Samia uchaguzi 2025

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema dhamira ya kweli ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuachia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani kuwa huru na haki.

Kinana ameyasema hayo leo Machi 5, 2024 katika Ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo unaoendelea kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Tunakwenda uchaguzi wa serikali za Mitaa, na mwakani uchaguzi mkuu mabadiliko matatu ya sheria yamefanyika, sheria ya uchaguzi, tume ya uchaguzi, vyama vya siasa,”amesema Kinana na kuongeza:

“Serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati mwaka huu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live