Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana akerwa kusuasua ujenzi barabara Kigoma- Kagera

Kinana Pic Data Kinana akerwa kusuasua ujenzi barabara Kigoma- Kagera

Fri, 2 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema kasi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayounganisha mikoa ya Kigoma na Kagera ni ndogo.

Kinana ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 2, 2022 akiwa eneo la Nyakanazi mkoa wa Kagera aliposimama akitokea mkoa wa Kigoma.

Mapema alfajiri, msafara wa Kinana ulitoka Kigoma kupitia wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko ambako ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami unaendelea.

Barabara hiyo imekuwa ikipigiwa kelele na wabunge wa mkoa wa Kigoma kwamba ujenzi wake hauendani na muda na umuhimu wake.

"Jumla ya wakandarasi watano wamepewa kazi hii ambayo inatarajia kuisha mwaka wa fedha ujao, kazi nzuri lakini siridhishwi na kasi ya ujenzi namna unavyokwenda," amesema Kinana.

Ziara ya Kinana leo inangia siku ya pili tangu alipoianza jana mkoani Kigoma ya kukagua miradi ya maendeleo na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020/25.

Akiwa Kagera atafanya vikao vya ndani na wanachama, kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi.

Kesho atahitimisha kwa mko wa Kagera kabla ya kuelekea Geita na kisha ziara hiyo ya siku tano atahitimisha mkoa wa Mwanza.

Chanzo: Mwananchi