Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana akemea viongozi wa CCM kuwadharau watendaji wa Serikali

KINANA CCM MKSZ Kinana akemea viongozi wa CCM kuwadharau watendaji wa Serikali

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea mtindo wa baadhi ya viongozi wa chama hicho kukejeli na kuwadharau watendaji wa serikali majukwaani, ikiwemo wakurugenzi huku kikisema wanafanya kazi kwa kuzingatia kanuni za utumishi.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho na Wajumbe wa Kamati Kuu za Siasa za chama hicho, Wilaya za Butiama,Bunda na Tarime mkoani Mara kwa nyakati tofauti, akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake, Makamu Mweyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amesema watumishi wa serikali wanastahili heshima zao kulingana na kazi wanazofanya.

“Mtumishi ni binadamu inapobainika amekosea haipaswi kuparamiwa kwenye mikutano ya hadhara, bali mifumo ya kiutumishi inapaswa kuzingatiwa katika kuwawajibisha na si utaratibu unaotumika wa kuwasema hadharani,” amesema na kuongeza:

“Tuache kuwasema, kuwakejeli wala tusiwadharau hao ni watendaji wa serikali na kuwasema wao maana yake unaisema CCM,…..heee wewe Mkurugenzi njoo hapa..,,, kimbia… simama hapo sema hivi …looh kisa! … jambo hili si sawa.”

“Wanastahili heshima yao na wana taratibu zao hawa, wana kanuni na wanaongozwa na kanuni na taratibu za kiutendaji, siajabu wakati mwingine mambo unayoyaagiza kwenye kanuni haipo, wala taratibu haipo popote, atakusikiliza atakwambia sawa, akirudi nyumbani anaenda kufanya shughuli zake zingine wala hakuzingatii,” amesema Kinana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live