Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana afurahishwa mwitikio wagombea CCM

Bcb984fb67fd2beae5e41875b05700ec.jpeg Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana

Sun, 7 Aug 2022 Chanzo: Habari leo

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema chama kinafurahi na kuridhishwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza kuwania uongozi katika ngazi mbalimbali.

Alisema hadi sasa mwenendo wa uchaguzi unakwenda vizuri na kwamba changamoto za hapa na pale hususani malalamiko, yatafanyiwa kazi na haki itatendeka. Kinana alisema hayo Dar es Salaam alipoungana na wana CCM wa Kata ya Oysterbay kuchagua viongozi wapya watakaokiongoza chama kwa miaka mitano ijayo.

“Yapo malalamiko ya hapa na pale, lakini nina hakika yatafanyiwa kazi ili mwanachama akishinda ashinde kwa haki. Msingi wa chama hiki ni kutenda haki, kwa hiyo nina hakika viongozi watatenda haki,” alisema Kinana.

Kinana aliyekuwa akiwasalimia wana CCM baada ya kukamilika kwa upigaji kura, alisema chama kinafurahishwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali na kufanya uchaguzi kwa amani.

Chanzo: Habari leo