Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana aeleza mkakati wa maridhiano nchini

Kinana Mkwaraaa Kinana aeleza mkakati wa maridhiano nchini

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameanza kazi kuleta maridhiano na mageuzi katika siasa na uendeshaji wa nchi.

Amesema kazi lengo ni kusimamia haki, kukuza, kuimarisha uhuru, kupanua wigo wa kuendesha shughuli za kisiasa utakaoleta mageuzi katika Serikali kwa madhumuni ya kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Kinana ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),amesema hayo wakati akifunga mkutano wa pili wa kumuenzi Maalim Seif aliyefariki dunia Februari 17 mwaka 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

“Hii si kazi rahisi kwani ziko changamoto zinazotukabili ikiwa ni pamoja na kutofautiana katika utekelezaji wake, kubisha kuhusu vipaumbele vyake na kuwa na mawazo tofauti kwa namna ya kasi ya utekelezaji wake.

“Nichukue fursa hii kuwasihi viongozi wenzangu wa vyama vyote kuendeleza ushirikiano katika kuchangia mawazo na kufanikisha amza hii ya Rais Samia. Tuendeleze utamaduni, kushauriana, kuvumialiana na kila mmmoja kuheshimu mawazo ya mwenzio licha ya tofauti zetu,” amesema.

Kuhusu Maalim Seif, Kinana amesema alikuwa kiongozi mwenye msimamo na subira na mwenye mapinduzi ya kweli. Pia Kinana amesema enzi za uhai wake, Maalim Seif alikuwa anapenda kuona vijana wanapata elimu bora inayoendana na mahitaji ya wakati yenye kuwajenga vijana kudadisi.

“Nilipata bahati ya kumfahamu Maalim Seif kwa miaka mingi iliyopita akiwa kiongozi ndani ya CCM. Hata alipohama CCM na baadaye kuwa makamu wa kwanza wa rais, haukuyumbishwa na tofauti za kimtazamo za vyama vyetu,” amesema Kinana.

Mmoja wa viongozi wa Taasisi ya Maalim Seif (MSF), Nassor Ahmed Mazrui amesema wakati wanamualika Kinana, kiongozi huyo hakufiria mara mbili kwenda katika mkutano huo.

Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, amesema watahakikisha wanaendelea kuandaa majukwaa kama hayo amabayo yatatoa michango mikubwa katika kuboresha elimu nchini kwa kuyashirikisha mashirika mbalimbali kutoa michango yao.

“Hii lililofanyika litakuwa endeelvu tutahakikisha tunatumia majukwaa kama haya kupata michango ya kuboresha elimu yetu, tuwashurukuru wote amabo wametuunga mkono kufanikisha hili kwa maslahi mapana ya taifa letu,” amesema Mazrui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live