Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinana: CCM siyo chama cha mtu bali ni mali ya watu

Cccmpic Data Makamu Mwenyekiti akifafanua kujimilikisha

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu mwenyekiti mpya wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema CCM siyo chama cha mtu ila ni mali ya watu.

Kinana ametoa kauli hiyo wakati akiwashukuru wajumbe waliompitisha kwa kura za asilimia 100 kwenye uchaguzi ambao alikuwa mgombea pekee.

Makamu huyo amesema siyo sawa kwa mwanaCCM kudhani kuwa chama hicho ni mali yake.

Amesema hakuna ukanda, udini wala ukabila bali wanaofanya hivyo ni wale walioishiwa hoja ambao hawakubaliki ndiyo ambao huingia kwenye kichaka cha ukabila, udini na uvisiwani.

Kinana ameahidi kusimamia haki na demokrasia ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika huku akieleza nia ya kuruhusu mawazo kwa wanachama.

"Lazima CCM kibaki kuwa sikio la Watanzania, tutajenga demokrasia ndani ya chama, tutatoka nafasi ya kumsikiliza kila mtu kwa nafasi yake, hayo yote tutafanya ili kutoa uhuru wa kidemokrasia kwa chama chetu," amesema Kinana.

Advertisement Amesema CCM ndiyo inapaswa kuisimamia Serikali siyo kwamba Serikali ndiyo itakisimamia chama kwani walioomba kura siyo Serikali bali ni chama.

Amesema ni wajibu wa chama kuikosoa Serikali pale inapobidi ingawa ukosoaji lazima uwe wa staha kwa kutumia njia za vikao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live