Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikwete: Kikosi kazi kitapunguza joto la kisiasa

Kikwete 1?fit=800%2C445 Kikosi kazi kitapunguza joto la kisiasa

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuunda kikosi kazi utasaidia kupunguza joto la kisiasa nchini na kutengeneza maridhiano.

Kikwete ameyasema hayo leo Ijumaa, Septemba 9, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa maoni yake mbele ya kikosi kazi cha kuratibu maoni kuhusu demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.

Kikwete aliwasili katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini hapa saa 4:07 asubuhi na kupokelewa na wajumbe wa kikosi kazi wakiongozwa na mwenyekiti, Profesa Rwekaza Mukandala, ametoka saa 12:10 mchana, akiwa ametumia saa mbili.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kikwete hakutaka kuweka wazi maoni yake mbele ya kamati, hata hivyo amesema amefurahi kupata nafasi hiyo na amempongeza Rais Samia kwa kuanzisha kikosi kazi hicho.

"Nampongeza Rais kwa kuunda kikosi kazi, ni uamuzi wa busara, utasaidia kupunguza joto ndani ya nchi na matumaini yake ni kwamba itasaidia kutengeneza maridhiano na mwenendo mzuri wa kufanya siasa hapa nchini," amesema Kikwete.

Kikwete ameungana viongozi wengine wastaafu ambao tayari wametoa maoni yao mbele ya kikosi kazi kuhusu namna bora ya kuimarisha demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.

Advertisement "Nimefurahi kupata nafasi ya kuja kwenye kikosi kazi," amesema Kikwete huku akisisitiza kwamba maoni yake ameyatoa kwenye kikosi kazi na siyo kwenye vyombo vya habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live