Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana anaelitaka Jimbo la Chenge afata fomu na Baiskeli

Screenshot 2020 07 17 At 13.46.55 660x400.png Joseph Bomani Nyanda, Mkazi wa Bupandagila Mkoani Simiyu

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Kijana Joseph Bomani Nyanda Mkazi wa Bupandagila Mkoani Simiyu amefika kwenye ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bariadi na kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Bariadi ambalo kwa miaka mingi limekua chini ya Andrew Chenge.

Tofauti na wengine ambao wamekua wakitumia magari wakati wanapokwenda kuchukua fomu, Nyanda ameamua kutumia usafiri wa Baiskeli na kusema hiyo inaakisi maisha ya Watu wa Bariadi.

Amesema “Nimefika hapa kuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa, tumeshuhudia wote namna Mwenyekiti wetu wa CCM anavyopambana usiku kucha kurudisha maendeleo kwa Wananchi, Mimi nimezaliwa kwenye hii Wilaya na usafiri wa awali kabisa kabla ya pikipiki na magari ilikua ni Baiskeli”

“Wakati nasoma Msingi na Sekondari nilikua natumia Baiskeli, hata wakati nakuja kuangalia matokeo yangu ya darasa la saba mwaka 2003 nilikuja kwa Baiskeli, hakukua na Pikipiki wala gari…. sasa lazima niakisi maisha niliyotokea huko nyuma katika mazingira ambayo nakwenda kuomba uongozi” – Nyanda

“Familia yangu ni familia duni, tumelelewa katika mazingira ya kutumia baiskeli, tunasomba maji na mazao shambani kwa kutumia baiskeli, na ndio usafiri uliotukuza…. tumemuona Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambavyo amekua akituasa mno namna ya kuenzi vitu vyetu vya asili, lazima tutembelee nyayo za Mwenyekiti wa Chama, na kiafya ni nzuri pia kujenga misuli” – Nyanda

Chanzo: millardayo.com