Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigwangalla: Nipo likizo ya kuongea

Kigwangallah Kigwangalla

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisi Andrea Kigwangalla; ni Mbunge wa Nzega-Vijijini mkoani Tabora ambaye jana kwenye mitandao ya kijamii kulisambaa nukuu yake yake tata iliyoibua mjadala mzito juu ya uongozi wa sasa uliopo madarakani nchini Tanzania.

Hata hivyo, leo, Kigwangalla ameibuka na kukanusha nukuu hiyo na kwamba yupo likizo ya kuongea akisema; “Jana @TanzaniaLeaks wameandika uongo. Nakanusha sijasema maneno hayo na wala huo siyo mtazamo wangu. Naomba @tcra_tanzania mchukue hatua stahiki dhidi yao.

Mimi nipo likizo ya kuongea na vyombo vya habari na mitandaoni si-post chochote, jimboni/bungeni sijaongea, wametoa wapi maneno hayo? CC: Mhe. @napennauye kwa hatua kali zaidi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live