Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo gani mwingine kung’oka Chadema?

96232 Kigogo+pic Kigogo gani mwingine kung’oka Chadema?

Wed, 19 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nani mwingine ataondoka Chadema. Ndilo swali unaloweza kujiuliza kutokana na waliokuwa wanachama wa chama hicho kukikimbia kwa nyakati tofauti, tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015.

Leo Jumanne Februari 18, 2020 aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amehamia CCM na kupokewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho tawala, Dk Vicent Mashinji.

Mwaka 2020 umeanza vibaya kwa Chadema.  imeshuhudiwa Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akihama Chadema na kurejea CCM na juzi aliyekuwa mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe naye alirejea CCM.

Sumaye alijiunga Chadema mwaka 2015 akitokea CCM na Mwambe akifanya hivyo mwaka huohuo baada ya kutoswa katika kura za maoni ndani ya CCM akiwania ubunge wa Ndanda. Alipotua Chadema alipewa nafasi ya kugombea na kuibuka na ushindi.

Leo Dk Mashinji aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema kuanzia Februari 2016 hadi Desemba 2019, baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza alieleza sababu za kukihama chama hicho kama zilizotolewa na Mwambe na Sumaye.

Swali la kujiuliza nani mwingine kung’oka Chadema, ni suala la muda tu.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumanne Februari 18, 2020 kujua walichokisema wabunge wanaotajwa kuhama Chadema

Chanzo: mwananchi.co.tz