Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Chadema asimamishwa kwa ubadhirifu

Kigogo Chadema.png Kigogo Chadema asimamishwa kwa ubadhirifu

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMATI ya Utendaji Kanda ya Magharibi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imemsimamisha uongozi aliyekuwa katibu wa chama hicho Mkoa Kigoma, Ismail Kangeta kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mikutano ya kampeni ya katiba mpya iliyoendeshwa na chama hicho mkoani Kigoma mwezi uliopita.

Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi CHADEMA, Gaston Garubindi alisema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma na kubainisha kuwa katibu huyo anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa Sh milioni 11 za chama hicho kwa ajili ya maandalizi ya mikutano ya kampeni ya Katiba Mpya ambayo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Freeman Mbowe na viongozi wa kitaifa wa chama hicho walikuwa wakiongea na wananchi.

Garubindi alisema kuwa kusimamishwa kwa katibu huyo ni hatua ya awali katika kuelekea kuchukua hatua zaidi kwa kiongozi huyo na tayari kamati hiyo ya utendaji ya kanda imetoa mapendekezo yake kwa Katibu Kuu ya Taifa ya CHADEMA kumuomba imchukulie hatua zaidi za kinidhamu.

Alisema kuwa Kamati ya Utendaji Kanda imemteua Ofisa wa Fedha na jimbo la Kigoma Mjini, Paul Jinery kukaimu nafasi ya Katibu wa Chadema Mkoa Kigoma hadi hapo utaratibu mwingine wa kujazwa kwa nafasi hiyo utakapofanywa.

Mwenyekiti huyo wa kanda ya Magharibi alisema kuwa pamoja na ubadhirifu huo wa fedha uliofanywa na kiongozi huyo mikutano kwa ajili ya kampeni ya Katiba Mpya iliyofanywa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu ambao waligawana makundi mawili ilifanyika na kuwa na mafanikio makubwa kulinagana na malengo yaliyowekwa kwenye kampeni hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live