Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo CCM: Hatuwezi kushinda uchaguzi kwa mabavu

Issa Gavu News Issa Gavu.

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Oganaizesheni, Issa Gavu, amesema chama hicho hakiwezi kushinda kwa kutumia njia za mabavu katika chaguzi, bali ili kishinde kinatakiwa kuandaa wagombea bora pamoja na kuhamasisha wananchi washiriki zoezi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Gavu ametoa kauli hiyo jana Jumanne, akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Shinyanga.

Katibu huyo wa organaizesheni CCM, alisema chama hicho kinapaswa kuandaa utaratibu wa kuwa na viongozi wawajibikaji, wanaojituma na kufanya kazi, ili waweze kuaminiwa na wananchi.

“Tunakwenda mwaka kesho utakuwa mwaka wa uchaguzi, njia pekee ya kuhakikisha kwamba chama chetu kinashinda ni kutengeneza utaratibu mzuri wa kuwa na viongozi wawajibikaji, wanaoweza kujituma na kufanya kazi. Hatuwezi kushinda kwenye mfumo wa vyama vingi kwa kutumia njia za mabavu,” alisema Gavu na kuongeza:

“Ili muende vizuri utakapofika wakati wa uboreshaji daftari la wapiga kura tuhakikishe tunahamasisha wanachama na wananchi wetu wajitokeze kwa wingi wakajiandikishe katia daftari ili ukifika wakati chama chetu kiwe na watu wengi waliojiandikisha ili mwisho wa siku kura zetu ziwe nyingi kuliko vyama vingine.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live