Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya wabunge wa Chadema yapigwa kalenda

99472 Pic+kesi+chadema Kesi ya wabunge wa Chadema yapigwa kalenda

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Kesi ya jinai inayowakabili wabunge wa Chadema na wenzao watano mkoani Morogoro imepigwa kalenda baada ya wakili wa jamhuri kuieleza mahakama kuwa kesi hiyo isogezwe mbele hadi Aprili 16, 2020 kwa ajili ya kusikilizwa wakati ikijiandaa kupeleka mashahidi.

Wabunge hao ni Peter Lijualikali (Kilombero) na Suzan Kiwanga(Mlimba) na washtakiwa wengine wa chama hicho.

Wakili wa Serikali, Calistus Kapinga alisema anaiomba mahakama isogeze mbele ili jamhuri iwe katika nafasi nzuri ya kuwaandaa mashahidi mahakamani hapo.

Kapinga alisema kuwa Aprili 16 mwaka huu watapeleka mashahidi dhidi ya washtakiwa katika kesi hiyo.

Wakili wa upande wa washtakiwa, Hekima Mwasipu akishirikiana na Jonathan Mndeme walisema kuwa shauri hilo ilipangwa leo Machi 18 kwa ajili ya kusikilizwa lakini upade wa jamhuri bahati mbaya haijapeleka mashahidi.

Wakili Mwasipu alisema kwa sababu sasa hivi kesi ipo mbele ya jamhuri, wameomba mahakama kuwasisitiza upande wa jamhuri kupeleka mashahidi ili kesi iendelee kusikilizwa.

Pia Soma

Advertisement

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Boniface Iyamwike amehairisha kesi hiyo mpaka AprilI 16 kwa ajili ya kusikilizwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz