Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kawaida: Tutawashughulikia wanaokejeli viongozi wetu

DBE9579A F458 412F BBFE 63C7CE73FC66.jpeg Mwenyekiti UVCCM, Mohamed Ali Kawaida

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Kawaida amesema watawashughulikia wanaowabeza viongozi wakuu wa nchi bila kujali nafasi zao walizo katika taifa hilo.

Ametoa kauli hiyo jana Desemba 10, 2022 katika ofisi za Jumuiya hiyo Gymkhana Mjini Unguja wakati wa mapokezi yake na kuwaagiza viongozi wote kuanzia ngazi za chini hadi taifa kushughulika na watu aliodai wanakejeli viongozi hao

"Viongozi mliochaguliwa, lazima tujue kwamba sisi ndio askari namba moja kuwalinda viongozi wetu wa taifa, hatutakubali kuona anajitokeza mtu yeyote anawakejeli viongozi wetu.

"Na hili niliseme wazi wenyeviti wa mikoa nawaagiza hakikisha hawa watu wanashughulikiwa, msipowashughulikia mimi nitawashughulikia ninyi," amesema.

Mbali na hilo amewataka viongozi hao ngazi za chini kutengeneza uchumi wa Jumuiya badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa ngazi zingine.

Naye Makamu Mwenyekiti , Rehema Sombi amesema wanapaswa kwenda na kasi ya Serikali huku wakizitumia fursa mbalimbali.

Awali Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenani Kihongosi amesema kazi hiyo ya kuongoza Jumuiya hiyo ni ngumu lakini itakuwa nyepesi iwapo watakuwa na ushirikiano.

Chanzo: Mwananchi