Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli za Polepole mitandaoni zaibua mjadala

95185 Pic+polepole Kauli za Polepole mitandaoni zaibua mjadala

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kauli za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kuhusu baadhi ya wananchi wa chama hicho aliodai kufanya mambo ya hovyo sambamba na kuvikosoa vyama vya upinzani imeibua mjadala mitandaoni.

Jana Jumapili Februari 9, 2020 Polepole aliendesha darasa la vijana wa CCM wa vyuo vikuu na vya kati jijini Arusha na baadaye kutumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter wa chama hicho kuwaponda makada wa chama hicho na wapinzani.

Polepole ametoa kauli hizo katika kipindi ambacho makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abulrahman Kinana na Yusuf Makamba wamekiweka katika mtego chama hicho tawala nchini Tanzania.

Ukimya wa kitu gani kinachoendelea juu yao unazidisha mjadala ndani ya chama hicho, baada ya taarifa ambazo hakuna upande uliozithibitisha iwapo wamejiuzulu uanachama wa CCM na kupo-teza sifa za kuhojiwa.

Taarifa za Kinana na Makamba kujiuzulu zimesambaa mitandaoni na Mwananchi limedokezwa kuwa barua zao za uamuzi huo wameziwasilisha ofisi ya katibu mkuu wa CCM zikiambatanishwa na kadi zao za uanachama.

 

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Alichokiandika Polepole baadhi ya wachangiaji wamekihusisha na sakata la kina Kinana na Makamba.

 

Katika ukurasa huo Polepole amesema, “wapinzani wanafanya siasa za madaraka na watafanya kila kitu hata mambo ya hovyo ilimradi wapate madaraka, ndio maana ukiwasikiliza vizuri wote hakuna anayezungumza mageuzi makubwa kwenye sekta ya ujenzi, afya na madini hawaoni chema chochote kinachofanyika kwenye Nchi yetu.”

“Ukizingua kwenye chama chetu hakuna mkubwa wala mdogo wote mnaitwa, ukikiimbia huna tofauti na wapinzani tu na watu wa hovyo kwenye chama chetu waondoke tu, wakiendelea kubaki kwenye chama chetu ni sumu.”

Ameongeza, “wakati Rais amemuagiza waziri mkuu kwenda kukagua makontena bandarini yupo kiongozi mkubwa wa chama sasa ni mstaafu alikuwa ana makontena 700 bandarini na hayajalipa kodi, alivyoambiwa alipe akaweka roho ya korosho, moyoni kanuna vibaya mno.”

Baadhi ya wachangiaji waliotoa maoni yao baada ya ujumbe huo wa Polepole walikuwa na maoni tofauti.

Malema Isere amesema, “ Tatizo ni moja wanaoambiwa hawana msingi na wapo madarakani sisi watanzania tunaona nchi inakwenda hata kama inatamba uhakika wa kufika upo, ila hao wanaomendea kuchukua nchi kabla hawajachukua maadili kwao ni 0 ni bora tutaendelea kutawaliwa na Baniani huyu kuliko jini lile.”

Naye Calvin Mbwambo amesema, “samahani sana kiongozi naomba usiwaite hao wazee ni watu wa hovyo maana wao ndo wamekufanya leo uwe na uone umuhimu wa hicho chama heshimu sana hao watu. Ipo siku yatakukuta haya yanayowakuta hutopata msaada take care brother.”

Kwa upande wake @dizzle254 amesema, “Daah maisha yanaenda kwa kasi sana aisee. Leo Polepole anamuita Kinana mtu wa hovyo…, aya  nyie endeleeni kutukana wazee wa chama halafu huko mbeleni tutaonana, hii ina onyesha jinsi gani chama chetu kwa sasa kipo mateka.”

“Hadi page (ukurasa)  ya chama mnaposti maneno yasio ya heshima kama haya. Hakika chama kipo kwenye mikono isiyo salama,” amesema @biljonie20.

“Yaani  hili nilikuwa nalitegemea sana na na nilijua 2020 kuna watu wakijiinua tu wamekwisha. Ukijua kucheza karata zako vizuri ahaa mambo yanaenda fresh tu. Kila kosa lina adhabu yake haijalishi ni la mwaka gani,” amesema Antweny Sawe.

Chanzo: mwananchi.co.tz