Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya kwanza ya Makonda baada ya kushindwa kwa kura Kigamboni

Screenshot 2020 07 21 At 10.23.01 660x400.png Kauli ya kwanza ya Makonda baada ya kushindwa kwa kura Kigamboni

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Tunafahamu matokeo ya kura za maoni kwenye Chama cha Mapinduzi CCM Kigamboni Dar es salaam jana Mshindi alitangazwa kuwa Dr. Faustine Ndugulile kwa kupata kura 190 kati ya kura 399 zilizopigwa huku Mshindi wa pili akiwa Paul Makonda aliyepata kura 122.

Wengi walikua na shauku ya kusikia chochote atachosema Mkuu huyu wa Mkoa wa Dar es salaam aliyepita Paul Makonda baada ya kutoshinda nafasi ya kwanza kwenye kura hizo za maoni ambapo leo Makonda ameyaandika haya.

“Nimepata pole nyingi sana kutokana na Matokeo ya jana, kwanza nawashukuru kwa upendo wenu na maombi yenu ya kunitakia mafanikio katika kutimiza NDOTO yangu”

“Jambo moja kubwa na muhimu ni kuyajua mapenzi ya Mungu na katika hili Mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu, nawatakia baraka na afya njema siku zote za maisha yenu”

“Asanteni sana sana wanakigamboni kwa upendo wenu na kunipa nafasi niwe sehemu ya Maisha yenu”Paul Makonda

Chanzo: millardayo.com