Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Dkt. Slaa kwa Freeman Mbowe

Dk Slaa 233 Balozi Dkt. Willibroad Slaa

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Balozi Dkt. Willibroad Slaa, amemtaka Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, aachane na masuala ya maridhiano na badala yake afanye siasa safi na kuwapatia wananchi katiba mpya.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 20, 2023, wakati wa mahojiano maalum aliyoyafanya kupitia kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio.

"Mbowe ni mzoefu wa siasa wa siku nyingi, ni mpambanaji, nikikutana naye nitamuambia afuate principal za siasa safi, simamia kwa sababu unatakiwa sasa hivi uwapatie Watanzania katiba mpya.

"Maridhiano hayafai kwa sababu yanakaa zaidi ya mwaka hakuna taarifa kwa wananchi, katiba inayodaiwa ni ya Watanzania si ya watu wawili," amesema Dkt. Slaa

Awali akizungumza amesema kwamba anao mchango mkubwa katika kukijenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA);

"Mimi ninajiona kama ninao mchango CHADEMA sina hakika kama watu wengine wanaona, kwa sababu baada ya miaka 20 ya kuwa Katibu Mkuu lazima utakuwa unajiona (Kama mchango anao ndani ya chama hicho),"- Dkt Slaa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live