Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Abdallah Bulembo kuhusu matendo ya Humphrey Polepole

Burembopiic Data Abdallah Bulembo,

Sun, 12 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti mstaafu wa jumuiya ya wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemtaka mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amwache Rais Samia Suluhu Hassan atekeleze majukumu yake.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 12,2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari akimjibu Polepole  kuhusu lawama alizotoa dhidi ya Samia ambaye ni mwenyekiti wa CCM.  

Bulembo amemuomba makamu mwenyekiti wa chama hicho bara, Philip Mangula kumuhoji Polepole kama alivyowahoji makatibu wakuu wa zamani, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba ambao sauti zao zilivuja wakikosoa viongozi na mwenendo wa chama hicho tawala, akitaka Polepole naye aitwe kamati ya maadili.

Huku akisisitiza kuwa anakemea suala hilo kama mwanachama wa kawaida na hajatumwa na mtu amesema, “kama Polepole anataka kutoka atoke atuachie CCM maana ana wenzake wanaomshawishi  kuanzisha chama chao,  asitapetape na kuongea mambo ambayo hayaeleweki.”

"Hawa kina Polepole waliojificha hawatusumbui ndani ya CCM kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama kama mwanachama anaenda tofauti kuna onyo, kufungiwa au kufukuzwa uanachama.”

Bulembo amesema anamfahamu Polepole  tangu mwaka 2012 alipoteuliwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete  kuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba.

Advertisement "Siyo kwamba ndani ya CCM tulifurahia uteuzi wake wa ukatibu mwenezi Taifa bali tuliheshimu mamlaka ya  aliyekuwa mwenyekiti Taifa hayati John Magufuli bali. Hamjali Samia na kimsingi hawezi kumpangia rais cha kufanya, yeye ni nani,”amesema Bulembo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live