Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mwenezi CCM apinga propaganda za uongo juu ya utekelezaji wa ilani ya CCM

Shakavvvf Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamidu Shaka

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna ahadi iliyotolewa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambayo haitatekelezwa ikiwemo mpango wa elimu bila malipo na utatuzi wa changamoto za sekta ya elimu nchini.

Amesema hayo wakati akikagua ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana Nachingwea iliyopo kata ya Chiumbati mkoani Lindi.

"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kugharamia elimu bila malipo. Ikiwa ni utekelezaji wa waraka wa elimu namba 6 wa mwaka 2015 na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025" Amesema Shaka

Aliwataka wananchi wapuuze taarifa zozote za upotoshaji zinazodai serikali itasitisha mpango wa kugharamia elimu bila malipo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live