Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu mpya  Bawacha aahidi makubwa

B434077d554c434208ba11fabdf5cf44.jpeg Katibu Mkuu mpya  Bawacha aahidi makubwa

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu mpya wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa (Bawacha), Catherine Rughe amesema baraza hilo litakulwa la kiwango cha juu na litasimamia utekelezaji wa mipango yake.

Rughe alisema hayo jana jijini Mwanza muda mfupi baada ya msimamizi wa uchaguzi, Ruth Mollel kumtangaza kushinda wa nafasi hiyo.

Mollel alisema Rughe alipata kura 34, mshindani wake wa karibu Ester Daffi alipata kura 23 na Asia Msangi kura nane.

Rughe aliwashukuru wajumbe wa Kamati Tendaji kwa kumuamini na kumchagua kuwa Mtendaji Mkuu wa Bawacha Taifa na kuwaahidi kuwa hatawaangusha.

Aliwashukuru wajumbe na wagombea wenzake na akaahidi ushirikiano kwa kuwa anatambua walikuwa na mikakati ya kulijenga baraza hilo.

Aliwataka viongozi wote waliochaguliwa wafanye kazi kwa kushirikiana ili kuliendeleza Baraza hilo kiutendaji katika viwango vya juu.

Kwa upande wa Zanzibar, mkutano huo wa Bawacha ulimchagua Bahati Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu ambaye alikuwa mgombea pekee na kupata kura 60 za ndiyo na tano za hapana.

Kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mollel alimtangaza Nuru Elias Ndosi kuibuka kidedea kwa kupata kura 33.

Mpinzani wake wa karibu, Brenda Rupia Jonas alipata kura 17 na Emma Bhoki alipata kura 15.

Mollel pia alimtangaza Aisha Machano Amme kuwa Mratibu Uenezi wa Bawacha baada ya kuibuka kidedea kwa kupata kura 36 na kumshinda Husna Said aliyepata kura 23.

Chanzo: www.habarileo.co.tz