Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu NCCR atimkia CCM

11423 Nccr+pic TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Danda Juju leo Jumamosi Agosti 11, 2018 amejiuzulu na kujiunga na CCM.

Danda amejiunga na CCM leo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya jamii wilayani Monduli.

Akizungumza na MCL Digital leo, Mkuu wa Idara ya Organaizesheni na Utawala wa NCCR, Florian Mbeo  amesema taarifa za Danda kuhama amezipata tangu leo mchana.

“Ni kweli ameondoka na tangu mchana nilijua jambo hili. Tulikuwa na taarifa zake maana leo asubuhi aliondoka na ndege kwenda Arusha akiwa na watu wa CCM,” amesema Mbeo.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu, Danda alikuwa msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho,James Mbatia. Alihamia NCCR akitokea Chadema.

Chanzo: mwananchi.co.tz