Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu CCM atoa siku 14 kwa kamati za Kisiasa

CHONGOLO12.jpeg Daniel Chongolo, Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM )

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM ), Daniel Chongolo ametoa siku 14 kwa kamati za siasa za wilaya na mikoa kuhakikisha zinapeleka taarifa za ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Chongolo amezitaka kamati hizo kuongeza juhudi katika kukamilisha kaguzi hizo huku akiwasisitiza kuwa ni wajibu kukamilisha jambo hilo ambalo sio la hiari.

"sisi tunawapa siku 14 wakamilishe hilo zoezi, hatuwezi kusubiria jambo moja, tumejiwekea utaratibu tutekeleze, hili jambo ni la wajibu na si hiari ni lazima na kila mmoja lazima alifanye".

Alihitimisha kwa kusema kuwa wao kama Sekretarieti wapo tayari kupokea taarifa hizo, ikiwa ni pamoja na kuweka msukomo kwakuwa wamepewa dhamana ya usimamizi na hawapo tayari kuonekana waongo kwasababu ya watu ambao hawajakamilisha zoezi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live