Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu CCM: Sensa isihusishwe na siasa

5ab83da6468f4e5170196ceb883b3d4f.jpeg Katibu Mkuu CCM: Sensa isihusishwe na siasa

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema masuala ya sensa yasihusishwe na mambo ya siasa kwani mipango ya nchi nyingi inaendana na takwimu ambazo zinaleta uchumi na maendeleo.

Pia amewataka viongozi mbalimbali wa CCM na serikali kuhakikisha katika mazungumzo yao na wananchi kuhamasisha kazi ya sensa iliyozinduliwa

juzi na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo linatarajia kufanyika mwakani.

Akizungumza wakati wa mapokezi yake akiambana na wajumbe wa Sekretarieti ya Taifa ya chama hicho katika Wilaya ya Lindi, Chongolo alisema bila ya kuwa na takwimu sahihi ya idadi ya watu kwenye eneo, huwezi jua mahitaji yao.

Alisema serikali ina utaratibu wa kufanya zoezi la sensa ya watu kila baada ya miaka 10. “Watu wengi wanakuja na kuhusianisha masuala ya sensa na siasa,” alisema Chongolo katika siku ya kwanza ya ziara

yake mkoani Lindi na katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Njombe.

“Sensa katika nchi ndio uchumi na ndio maendeleo, tukitengeneza mazingira mazuri tunahamasishana na kujitokeza vya kutosha katika kushiriki sense, zoezi ambalo limezinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana (juzi) Dodoma.”

Aidha, Chongolo alisema watu watakapohamasika na kujitokeza katika sensa, nchi itakuwa imejisaidia katika mipango yake na watu wakihesabiwa kwa nidhamu itasaidia kuleta maendeleo katika nchi.

“Viongozi kila mmoja arudi kwenye eneo lake maandalizi ya zoezi la sensa 2022 yawe sehemu ya mazungumzo yenu kila siku, nendeni mkajiandae sensa ina tija,” alisema mtendaji huyo wa CCM.

Aidha, aliwataka wanaofuatilia nafasi za ubunge na udiwani waaache mara moja kwani CCM ina macho ya marefu, inaona mbali na hakuna mtu atakayeachwa kwani muda huu ni wa wabunge na madiwani kufanya kazi kwani uchaguzi umeshapita; na CCM hakiwezi kuwa chama cha uchaguzi wakati wote

badala ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Alisema watu hao wanapaswa kuwaacha wabunge kufanya kazi kwani chama chao kina mifumo na kazi yake ni kuhakikisha kinaongoza na kutoa uongozi.

“Kama unapenda ubunge ama udiwani subiri 2025, sasa hivi chokochoko katika majimbo yanatoka wapi, na chokochoko za nafasi zinatoka wapi? Waacheni wabunge wafanye kazi wanavyofanya subiri 2025 tukiangaika kuwafuatilia sasa hivi na kuwazushia tutafika mwaka 2025 na

majeraha makubwa badala ya kutafuta ushindi taratibu majeraha hayo ambayo si sawa,” alisema Chongolo.

Chongolo alisema katika Uchaguzi Mkuu wa ndani wa chama unatarajia kufanyika mwakani, na kwamba mtu akitaka kuchaguliwa kuwa kiongozi ndani ya CCM ni lazima awe amehudhuria mikutano ya mashina.

Pia aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi na maeneo mengine kuwekeza bidii ya kusomesha watoto wa kike na kuondokana na fikra za watoto hao kuolewa tu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz