Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katiba mpya yatawala mdahalo Bavicha

Katibapic New Mdahalo wa Baraza la Vijana CHADEMA

Sun, 22 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hoja ya madai ya Katiba mpya imetawala katika mdahalo wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) mkoa Arusha huku mkutano wa jana wa Rais Samia Suluhu na viongozi wa Chadema ukitajwa ni safari ya kupata Katiba mpya.

Jana Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na viongozi wa juu wa Chadema na CCM Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Akizungumza katika kongamano hilo leo Jumamosi Mei 21, 2021, Katibu Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema wanaamini Rais Samia amepata ujumbe wao.

"Rais kukutana na viongozi wetu wa ngazi za juu tunaowaamini, kimetupa kiburi mpya cha kutembea kifua mbele kudai Katiba mpya maana tunaamini moja ya ajenda walichozungumza ni mchakato wa Katiba mpya ambao umekuwa ajenda yetu tangu uchaguzi uliopita" amesema

Golugwa amesema kuwa wanaanza harakati upya kuhakikisha Katiba mpya inapatikana kwani wanaamini ndio mkombozi wa maendeleo ya nchi.

"Makamanda tuamke kudai Katiba mpya kwa harakati zote bila kujali kwa mikutano au maandamano naomba mjitokeze kila tutakaotangaza kwani mafanikio hayo ni faida kwa watoto wetu na vizazi vijavyo"amesema

Kwa upande wake aliyewahi kuwa mgombea ubunge Jimbo la Namtumbo, Zamda Ngonyani aliwataka vijana hao waanze kujitokeza kwa wingi bila kujali kadhia wanazopitia.

"Tumefilisiwa wengi hasa biashara zetu na uwekezaji mkubwa tuliofanya hasa viongozi wa juu lakini tuhamie sasa kwenye kilimo, kule kwetu Ruvuma tunalima mazao mengi kama korosho, kahawa na matunda mengi hivyo hata tukifilisiwa biashara lakini ardhi haitatutupa tuendelee na harakati tusirudi nyuma na kazi pia za kiuchumi tufanye kwa bidii" amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live