Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kata ya Yusuph Manji yatafutiwa mrithi

10799 Manji+pic TanzaniaWeb

Wed, 8 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam.Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imetangaza uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 21 za mikoa 10 ya Tanzania Bara na Visiwani ikiwamo Mbagala Kuu ambayo ilikuwa ikiongozwa na mfanyabiashara Yusuph Manji.

Mkurugenzi wa Nec, Dk Athuman Kihamia ameyasema hayo jana Agosti 7 wakati alipotangaza kata za udiwani katika uchaguzi mdogo wa Septemba 16 mwaka huu.

Dk Kihamia ametangaza uchaguzi huo baada ya kupokea taarifa ya uwepo wa nafasi 21 zilizopo katika halmashauri 15 kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo.

Uchaguzi huo mdogo utakwenda sambamba na ubunge katika majimbo matatu ambayo ni Korogwe vijijini, Ukonga na Monduli .

“Nafasi za udiwani katika kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali ikiwamo kifo, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama,” amesema Kihamia.

Dk Kihamia amesea fomu za uteuzi  wa wagombea wa uchaguzi huo zitatolewa kati ya Agosti 17 hadi 23 mwaka huu na uteuzi utafanyika Agosti 23 mwaka huu wakati kampeni za uchaguzi zitafanyika kati ya Agosti 24 hadi Septemba 15.

Soma Zaidi:

Manji afunguka mahakamani kuhusu kuvuliwa udiwani

 

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz