MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza,kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dk Angelina Mabula amewahidi wakazi wa kata ya Ilemela kuwa atawaboreshea miundo mbinu ya barabara katika kata hiyo.
Dk Mabula alitoa rai hiyo wakati wa mkutano wa kampeni katika viwanja vya Isenyi. Dk Mabula alisema tayari Serikali ya CCM imetenga shilingi milioni 83 kwajili ya ujenzi wa barabara ya Lumala-Pasiansi, barabara ya Kiseke-Lumala imetengewa milioni 39/-
Alisema Barabara hizo zitajengewa lami pamoja na kuwewa taa. Katika sekta ya ardhi alisema jumla ya viwanja 534 vimepimwa na wakazi waliochukua hati kutoka Lumala ni 317. Dk Mabula alisema katika Afya,Serikali ya CCM jumla ilitoa milioni 900 kwajili ya ukarabati wa vituo vya afya vya Karume na Buzuruga
Aliahidi kuhakikisha anawawekea umeme wakazi Igogwe katika kata ya Bugogwa. Alisema katika kero ya maji tayari,Serikali imeanza ujenzi wa mabomba ya maji na tayari usambazaji wa mabomba unaendelea. Alisema katika sekta ya Elimu,Serikali imetenga milioni 120 kwajili ya kujenga madarasa matatu katika shule ya sekondari Kisunzu,madarasa mawili katika shule ya msingi Isanzu na darasa moja katika shule ya msingi Igombe.
Mgombea udiwani wa kata ya Bugogwa kupitia CCM,Mashamba William aliahidi atashirikiana na mbunge wa Ilemela Dk Angelina Mabula katika kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Igogwe.