Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karamagi ashinda Uenyekiti wa CCM Kagera

Naziri Karamagi.jpeg Naziri Karamagi

Wed, 23 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Naziri Karamagi ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera baada ya kupata kura 669 sawa asilimia 58 ya kura zilizopigwa.

Karamagi ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini mwaka 2005-2010, aliwabwaga, Costansia Buhiye alipata kura 452, Medard Mushobozi kura 18 na Novath Kwama kura 5.

Msimamizi wa Uchaguzi huo, Dk Tulia Ackson alimtangaza Karamagi pamoja na mshindi wa nafasi ya uwakilishi katika Halmashauri Kuu ya Chama, Kareem Amri.

Dk Tulia amesema Amri amepata kura 751, akiwaangusha Wilbroad Mtabuzi ambaye amepata kura 368 na Amani Kajuna aliyepata kura 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live