Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni yaanzishwa kumpinga Mtatiro mitandaoni

11417 Hashtag+pic TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watumiaji wa mitandao ya kijamii waliokuwa wakimfuatilia mwanasiasa Julius Mtatiro katika mitandao yake ya kijamii wameanzisha ‘hashtag’ ya kutomfuatilia mitandaoni (unfollow) mwanasiasa huyo ikiwa ni saa chache baada ya kutangaza kuhama CUF.

Si kawaida kwa wafuasi kuanzisha kampeni za kuacha kuwafuata wanasiasa kwenye mitandao yao mara baada ya kujiunga na vyama vingine.

Mtatiro aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya CUF, alitangaza kujiunga CCM leo Agosti 11.

Hashtag hiyo ya;  #unfollowMtatiro# na #BlockMtatiro# imeanzishwa na wale walioonekana kukasirishwa na uamuzi wa Mtatiro wakiongozwa na  Mtanzania aishiye nje ya nchi, Evarist Chahali, ambaye ni mtumiaji mkubwa  wa mitandao ya kijamii.

Soma Zaidi:

Bashe, Nape, Zitto, Polepole wajadili kuondoka Mtatiro CUF

Chahali, anayetumia akaunti ya twitter @Chahali, ameanzisha kampeni hiyo na kuhimiza wafuasi wengine kuacha kumfuata Mtatiro, kwenye mitandao ya facebook, twitter na instagram

Mtumiaji mwingine wa twitter, AIDAN JR (MARLEY) mwenye akaunti ya twitter ya @ajGOODKID naye amejumuika katika kampeni hiyo.

“Nimelazimika kufanya hivi kwa kweli,” ameandika Aidan.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz