Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni ya wabunge yahamia Dar

14186 Pic+wabunge TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Chama cha wabunge wanawake Tanzania, kitaendelea na kampeni yake ya kuchangua ujenzi wa vyoo bora katika shule za sekondari na za msingi jijini Dar es Salaam.

Kampeni hiyo inayotarajiwa kufanyika kwa njia ya tamasha, itafanyika Ijumaa  ijayo Agosti 31.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, makamu mwenyekiti wa kamati ya uendeshaji wa kampeni hiyo, William Ngeleja amesema wamepanga tamasha hilo lifanyike kwenye ukumbi wa Mlimani City.

 

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuhakikisha wanakusanya Sh3.5 Bilioni ili kufikia ujenzi wa vyoo bora vya shuleni.

Amesema awali lilifanyika Jijini Dodoma na walifanikiwa kukusanya fedha taslimu na ahadi Sh1.4 bilioni.

Na safari hii  wameamua kufanyia Dar es Salaam wakiamini watafikia lengo walilokusudia.

“Kama tulivyofanya Dodoma, vivyo hivyo tutakavyofanya hapa, hivyo niwatake Watanzania wasikose kushiriki katika tukio hilo muhimu, wao ni wadau muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapa huduma nzuri ya vyoo bora shuleni.

“Katika tamasha hilo tutakuwa na matukio ya burudani mbalimbali kama sarakasi, taarabu, kwaya maalumu, shairi, maigizo na muziki wa kisasa, vyote hivyo vitatolewa na wabunge wenyewe,” amesema Ngeleja.

Chanzo: mwananchi.co.tz