Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni uchaguzi wa serikali za mitaa kuanza kesho

84622 Pic+kampeni Kampeni uchaguzi wa serikali za mitaa kuanza kesho

Mon, 18 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Nyamuhanga amesema maandalizi ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zitakazoanza kesho yanakwenda vizuri na kuwa mchakato huo hautafanyika katika maeneo ambayo wagombea wamepita bila kupingwa.

Mbali na hilo, Nyamuhanga amesisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na vitongoji hautafutwa kwa mujibu wa kanuni.

Nyamuhanga ameeleza hayo leo Jumamosi Novemba 16, 2019 wakati akizungumzia mwenendo wa uchaguzi huo na kampeni zitakazoanza kesho Novemba 17 na kuhitimishwa Novemba 23.

Amesema kwa takwimu za awali, katika vijiji 12, 319 wagombe 6,837 sawa na asilimia 55 wamepita bila kupingwa, katika ya mitaa 4,263 wagombea 1,279 sawa asilimia 30 wapita bila kupingwa na katika vitongoji 64,384 wagombea 4,207 sawa asilimia 62 wamepita bila kupingwa.

"Maeneo yote ambayo wagombea wamepita bila kupingwa hayatakuwa na shughuli za kampeni. Awali tulikuwa na vituo vya kupigia zaidi ya 100,000, lakini vitapungua kutokana wagombea kupita kupingwa na wengine kujitoa katika mchakato huu.

"Bado tunaendelea kuhuisha takwimu za wagombea  waliojitoa kwenye mchakato huu na tutazitoa kwa umma. Nawaomba wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kusimamia kwa ufanisi wa kampeni wakishirikiana na jeshi la polisi litakaloimarisha ulinzi," amesema Nyamuhanga.

Amefafanua kuwa katika mchakato huo, vikundi vya ulinzi binafsi na vya jadi na vile vya mashabiki wa vyama husika havitaruhusiwa kushiriki kwenye ulinzi katika kampeni hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz