Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kambi ya Maalim Seif yaendelea kutangaza vita kwa Profesa Lipumba

45975 Pic+cuf Kambi ya Maalim Seif yaendelea kutangaza vita kwa Profesa Lipumba

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku moja baada ya kambi ya Maalim Seif kutangaza kuzuia mkutano  uliopangwa kufanyia na kambi ya Lipumba wenye lengo la kumfukuza Maalim Seif uanachama, wanachama wa chama hicho kata ya Azimio wamesema wanaunga mkono tamko la katibu mkuu huyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Machi 10, 2019 na wanachama wa kata ya Azimio wilayani Temeke walipokutana kujadili tamko lililotolewa na Katibu Mkuu Maalim Saif la kutaka mkutano huo kuzuiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama katibu wa kata hiyo, Rajabu Matata amesema wanapinga kwa nguvu zote mkutano feki wa Lipumba anaouita mkutano mkuu wa taifa unaotokana na wajumbe feki.

"Sisi tukiwa wanachama tawi la Be Care hatujawahi kuona uchaguzi unaendeshwa kwa ngazi ya matawi, kata au wilaya kwa lengo la kupata wawakilishi wa taifa," amesema Matata.

Amesema wanataka utaratibu ufanyike kama unavyofanyika kwa miaka yote na kuviomba vyombo vya dola kuzuia mkutano huo feki, wasipofanya hivyo viongozi na wanachama watahakikisha wanatumia njia wanazozijua wao.

Hassan Malenga ambaye ni mwanachama wa tawi la Be Care amesema maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu Maalim Seif wameyapokea na wameanza kuyatekeleza kukabiliana na wajumbe feki wa mkutano huo.

"Mkutano ulioandaliwa na Lipumba ni hewa na ni genge la wahuni, tumejipanga kukabiliana nao, tumeshapokea maelekezo kutoka kwa katibu mkuu wetu yatakayotokea tusilaumiane," amesema Malenga.



Chanzo: mwananchi.co.tz