Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya kudumu ya Bunge ya PIC yaipongeza STAMICO

Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya PIC Yaipongeza STAMICO.jpeg Kamati ya kudumu ya Bunge ya PIC yaipongeza STAMICO

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imetembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo jijini Mwanza na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Ndugu Deus Clement Sangu imeona maendeleo mazuri ya usafishaji wa dhahabu kiwandani hapo ikilinganishwa na kipindi cha nyuma walipotembelea kiwandani hapo

Aidha Mwenyekiti wa Kamati ameipongeza Serikali kupitia STAMICO kwa kuongeza mapato yake pamoja na kuanzisha kiwanda hicho ambacho kitapelekea STAMICO kupata mapato na nchi kupata faida mbalimbali kutokana na usafishaji wa dhahabu nchini

Katika wasilisho lake la kamati Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Dkt Venance Mwasse alielezea utekelezaji wa shughuli za kiwanda pamoja na changamoto ya kiwanda ya kutokupata dhahabu ghafi kwa wingi kutokana na maswala mbalimbali ikiwemo changamoto ya kikodi.

Kamati iliahidib kuifanyia kazi changamoto hii ya kikodi kwa kushirikiana na Serikali ili kiwanda kiweze kupata malighafi ya kutosha na kufanya kazi vizuri

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo aliishukuru kamati ya PIC kwa ushauri wao wanaoutoa mara kwa mara kwa Shirika kuhusu maswala ya uwekezaji nakupelekea Shirika kuendelea kufanya vizuri

Ziara hii ya Kamati itahusisha kutembelea miradi mingine ya Shirika ya STAMIGOLD na Makaa ya mawe Kiwira ili wajumbe wajionee uwekezaji wa STAMICO katika miradi mbalimbali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live