Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati Kuu ACT-Wazalenzo yajifungia kuandaa mkutano mkuu

Kuu Pic Data Kamati Kuu ACT-Wazalenzo yajifungia kuandaa mkutano mkuu

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Chama Cha ACT-Wazalenzo kimeanza kufanya kikao cha Kamati Kuu kuandaa agenda kuelekea kwenye mkutano wa halmashauri Kuu unaotarajiwa kufanyika kesho Januari 28, 2022 ikiwa ni maandalizi ya mwisho ya mkutano mkuu utakaofanyika Januari 29.

Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho mkutano mkuu unafanyika kila baada ya miaka mitano lakini baada ya kufariki dunia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, imelazimu chama hicho kufanya Mkutano huo ili kuchagua atakayeziba nafasi hiyo na kuzingatia Sheria ya Vyama vya Siasa.

Maalim Seif alifariki dunia Februari 17 mwaka jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Baada ya kumaliza mkutano wa Halmashauri Kuu kesho ambao utapitisha majina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa halmashauri Kuu wanategemea kuingia kwenye mdahalo wa wazi kwa wagombea kueleza malengo yao endapo watapata nafasi wanazogombea.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho kinachofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho, Dorothy Semu  amesema anaamini wajumbe waliojitokeza kushiriki mkutano huo watatoa uwakilishi mzuri.

"Hoja zitakazo saidia kutekeleza mikutano miwili wa Halmashauri Kuu unafanyika kesho na Mkutano Mkuu maalumu wa kuchagua viongozi wetu keshokutwa Jumamosi," amesema Dorothy

Wagombea wanaowania nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa wako wawili ambao ni  Juma Duni Haji  na Masoud Hamad Masoud huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikiwaniwa na  Othuman Masoud Othuman na  Juma Said Sanani.

Katika nafasi  moja ya ujumbe wa Halmashauri Kuu inagombewa na watu saba kwa sababu mwanachama aliyepungua ni kutoka Tanzania Bara ambao ni Joseph Msipi, Esta Thomas, Fungo Benson, Johnson Mauma, Msafiri Ntemerwa, Japhet Massawe na Fidelini Hemed Christopher

Chanzo: www.mwananchi.co.tz