Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalima ataka viongozi CCM kuvunja makundi

Makundi Kalima CCM.jpeg Kalima ataka viongozi CCM kuvunja makundi

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: Mwananchi

Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi CCM, Gilibert Kalima amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho kuvunja makundi yaliyotokana na kampeni za uchaguzi wa ndani wa chama hicho tawala.

Ameyaeleza hayo jana Jumatatu Oktoba 10, 2022 wakati akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, “wito wangu ni kuvunja makundi yote yaliyotokana na kampeni zote za uchaguzi wa CCM, ili tuweze kufanya vizuri zaidi kwani tumekuwa na tabia mbaya ya kuhamisha makundi. Tunatakiwa kuyaondoa kwa sababu yakiendelea kuwepo ni hatari kubwa.”

"Najua Shinyanga yapo makundi lakini tufike mahali tuyavunje na tuseme hapana ili tusipotoshe wananchi wetu ambao tumechukua jukumu la kuwatetea, msichukue jukumu la kumpinga mtu.”

Amewataka viongozi kuwa makini na wanaopanga safu kwa sababu watu hao ni hatari ndani ya chama, “unakuta madiwani na wabunge wanapanga safu yao kuanzia mashina, kufanya hivyo ni hatari kwa uhai wa chama, badala yake wasimame vizuri kwenye vikao vya tathimini ili waendelee kuwa na chama bora cha kuaminiwa na wananchi.”

Kalima amesema wenyeviti wa mitaa na vijiji wanatakiwa kufanya mikutano baada ya miezi mitatu, kama hawafanyi wanatakiwa kukumbushwa.

Chanzo: Mwananchi