Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalanga aanza rasmi kuibomoa Chadema

10190 KALANAGA+PIC TanzaniaWeb

Sun, 5 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Aliyekuwa mbunge wa Monduli kupitia Chadema, Julius Kalanga ambaye amejiuzulu na kujiunga na CCM, amewataka vijana katika Jiji la Arusha kujiondoa Chadema kwa madai kuwa hakuna uwezekano wa chama hicho kushika dola.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni Kata ya Kaloleni jana, Kalanga alisema hakuna sababu ya kukaa katika chama ambacho hakiwezi kushika dola.

“Kama mimi mbunge wa Monduli nimeondoka na mnajua Monduli ilivyo, nyie hapa mnasubiri nini?” alisema.

Alisema ukiwa upinzani si rahisi kupata misaada na ushirikiano na serikali jambo ambalo amelibaini na kulifanyia kazi.

“Hata kama una hoja nzuri haisikilizwi, mimi ndiye nilianza hoja kupinga watu waliokosa vyeti vya kidato cha nne kufukuzwa kazi lakini sikusilizwa hadi alipoongea (Joseph Kasheku) Msukuma ndipo serikali ikachukua hatua,” alisema

Alisema ni ‘uboya’ kubaki kuwa upinzani ambapo hata ukipata matatizo hakuna mtu wa kukusaidia.

“Nawaomba Arusha msifanye makosa chagueni wagombea wa CCM,” alisema Kalanga. Katika kata hiyo ya Kaloleni, Kalanga aliomba wananchi wamchague mgombea wa CCM, Emmanuel Kessy kwa kura nyingi.

Awali Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kama Msukuma, alimtaja Kalanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz