Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalanga, Musukuma wamshukia Lowassa

15167 Pic+kalanga TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Wakati mbunge Joseph Kasheku maarufu Musukuma amesema enzi za Edward Lowassa zimekwisha, mgombea wa CCM jimbo la Monduli, Julius Kalanga amemtaka waziri mkuu huyo wa zamani aache kumdhalilisha.

Musukuma ambaye ni mbunge wa Geita Vijijini (CCM), wakati akimnadi Kalanga kwa wakazi wa eneo la Mto wa Mbu aliwataka wananchi hao kumsahau Lowassa kwani amekwisha na hawezi tena kutatua kero zao.

Kuhusu madai yaliyotolewa na Lowassa kuwa Kalanga ameshindwa kulipa deni la Sh600 milioni, alisema sio jambo la ajabu kudaiwa.

“Mbunge anaweza kukopa na kama kweli ng’ombe zilikufa mbona yeye (Lowassa) amezificha huko lanchi zisife na kilimo kama hakufanikiwa ni sawa na wananchi wengine, hivyo sio ajabu,” alisema Musukuma.

Musukuma alisema, Kalanga ameacha mshahara wake, miaka miwili, ili aje kushirikiana na wabunge walio wengi kutatua kero za wananchi kwa sababu haliko kuwa haikuwezekana kuzitatua.

Akijinadi kwenye mkutano huo, alisema amesikitishwa na kauli za Lowassa, mzee ambaye amemuheshimu kwa zaidi ya miaka 20, kutoa maneno ya uongo hadharani na kumdhalilisha.

“Nimewaambia wazee wa kimila waone huyu mzee jinsi ambavyo hanitendei haki kwa sababu tu mimi ni masikini, anasema uongo kuwa nimejiuzulu ubunge baada ya kushindwa kulipa deni la milioni 600,” alisema.

Kalanga alisema vijana zaidi ya 50 wa Chadema wamekasirishwa na kauli za Lowassa na wame amua kukihama chama hicho na kujiunga CCM.

Alimuomba Lowassa apumzike kwani amemaliza muda wake, awaachie vijana wa Monduli waendelee kusaidia wananchi.

Chanzo: mwananchi.co.tz