Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakunda alipigia debe zao la muhogo

50637 Pic+kakunda

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imetaja vipaumbele vitatu ambavyo vimewekewa msisitizo wa uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda ameliambia Bunge leo Ijumaa April 5, 2019 kuwa katika vipaumbele hivyo ni pamoja na kuliangalia kwa karibu soko la muhogo ambalo limekuwa kubwa duniani.

Kakunda ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mussa Mbarouk (Tanga Mjini- Cuf) ambaye alitaka kujua Serikali ina mkakati gani kutafuta soko la uhakika la zao la muhogo pamoja na kuomba Serikali kuondoa kodi katika mashine za kusindika mazao hayo.

Waziri ametaja vipaumbele vya Serikali kuwa ni ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, viwanda vya kutengeneza bidhaa za majumbani na vile vinavyoajiri watu wengi.

Amesema zao la muhogo limepewa kipaumbele maalum duniani kutokana na ongezeko la matumizi yake ikiwemo kuunganishia vyuma na kutengenezea gundi na kuongeza kuwa China pekee kwa sasa inahitaji tani milioni mbili na nusu kwa mwaka.

Kuhusu gharama za vifaa amewataka wawekezaji kuanza kuangalia vifaa vinavyotengenezwa na Sido badala ya kuagiza vifaa vya nje.



Chanzo: mwananchi.co.tz