Thu, 30 May 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki akimpa chakula mtoto wa tembo katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Mei 30, 2024.
Wizara hiyo imeamua kuleta baadhi ya wanyama pori akiwamo simba, tembo, kobe na duma kwa ajili ya kuhamasisha wabunge, watumishi wa Bunge na wageni mbalimbali wanaotembelea bungeni.
Kesho, Kairuki anatarajiwa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024 / 2025.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live