Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadi za CCM zanaswa zikisambazwa kinyemela Buchosa

Ccmpiic Data Makoye amesema wanachama wasio waaminifu wamefanya hivyo

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kimebaini kusambazwa kinyemela kadi za chama hicho bila kufuata utaratibu na baadhi ya wanachama wasio waadilifu.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema, Marco Makoye amewaambia waandishi wa habari kuwa kadi hizo zimekamatwa kata ya Nyakarilo jimbo la Buchosa na zingine zimekamatwa kata ya Busisi jimbo la Sengerema.

Amesema CCM inautaratibu wake wa kutoa kadi hizo kwa wananchama.

Kufuatia hali hiyo, amesema wametuma taarifa makao makuu ya chama katika kitengo cha Tehama kujua kadi hizo kama zimesajiliwa na kubaini aliyezichukuwa pamoja na kuzisamba kwa wananchama bila utaratibu.

"Utaratibu wa kuagiza kadi unafanywa na ofisi ya chama wilaya na hakuna mtu aliye na mamlaka ya kuagiza kadi, hivyo mwanachama yeyote atakaye bainika kufanya jambo hilo bila kujali cheo chake atawajibishwa kwa mujibu wa kanuni za chama," amesema Makoye.

Mmoja wa mwananchama wa CCM wilayani humo, John Mathias amesema kuzagaa kwa kadi hizo bila utarabu, chama kinatakiwa kuchukuwa hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live