Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate awataka vijana kutotumika

Wazazi Msikwepe Jukumu La Malezi Ya Watoto   Jokate Jokate awataka vijana kutotumika

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Jokate Mwegelo amewataka vijana nchini kutotumika katika vitendo ambavyo vitasababisha kuvunjika kwa amani pamoja na kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii.

Jokate ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa UVCCM uliofanyika katika Mtaa wa Shilabera Mjini Geita, ambapo amewataka viongozi wa chama na Serikali ngazi ya mkoa kote nchini kuanza kuwatambua vijana wenye uwezo ambao watakuwa na uwezo wa kuongoza Serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa Serikali za Mitaa.

"Ujumbe wetu wa kwanza tunataka kuwahimiza vijana wote hususani vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokubali kutumika vibaya, vijana tusinunuliwe, vijana tujitambue tujue tuna fursa kubwa chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan", amesema Jokate

Chanzo: www.tanzaniaweb.live