Ndiyo ni sahihi kusema hivyo kuhusu Jokate Mwegelo. Mengine yote yamefanywa zaidi yake na wengine ambao wangeweza kupata nafasi aliyonayo hivi sasa. Elimu, umaarufu, kujuana na watu na kukipenda chama. Ana bahati sana Jojo ndio ukweli.
Pamoja na bahati lakini anastahili. Vyovyote iwavyo ana tofauti kubwa na wasanii wengi. Hata kama samaki mmoja akioza wote wameoza kuna mmoja atakuwa na nafuu kwa kitoweo. Jokate anastahili na Mungu ampe nguvu.
Somo kwa wasanii wasioangalia kesho yao. Wanaogeuza ngozi zao kama kuta za gereza kwa maandishi (tattoo). Wanaobeba ya vyumbani, nyumba za wageni na kutundika mitandaoni. Mtaongoza watu 'lokesheni' siyo UWT. Nani awateue?
Usanii siyo kuishi ovyo ovyo. Siyo kubadaili wapenzi na kujichetua mitandaoni kwa picha za utupu. Mtazameni Jokate kama taa yenu. Ukijihehsimu na kujiendeleza kielimu utatoboa tu.