Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate Mwegelo anavyoaminisha madaraka kwa vinana

Jokate Mwegelo Mkj Jokate Mwegelo anavyoaminisha madaraka kwa vinana

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kambi ya Miss Tanzania mwaka 2006 ilikuwa moto wa kuotea mbali. Wakati huo shindano hilo lilikuwa la moto kweli kweli, kwa wale waandishi wa habari za urembo walilibatiza jina la Sikukuu ya Krismasi ama Iddi, ilikuwa kazi, wakati huo huo mtoko.

Hiyo ilitokana na unyeti na umaarufu wake, lilikuwa ndio shindano ambalo kwa miaka hiyo kiingilio kilikuwa Sh 100,000 na bado tiketi ziliisha na wapenzi wa urembo walilalamika kukosa, hawakulalamikia kiingilio.

Pengine hakujatokea na hakutatokea shindano lililokuwa kali na lenye upinzani mwingi kwenye tasnia ya urembo kama la mwaka huo.

Hilo linajidhihirisha mpaka sasa kwani warembo waliowania taji kwa mwaka huo wakiongozwa na Wema Sepetu aliyeibuka mshindi, mpaka sasa hawapoi, wako midomoni mwa jamii ya Tanzania wakihusishwa na masuala mbalimbali yanayoizunguka jamii.

Tano Bora ya Miss Tanzania mwaka 2006 ilikuwa Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Lisa Jensen, Sara Kagenzi na Irene Uwoya.

Ukiona majina hayo, nadhani unapata picha shindano la mwaka huo chini ya Hashim Lundenga (anko) lilivyokuwa.

Huko ndipo nyota ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jokate, ilipoanza kung’ara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live