Spika Mstaafu wa Bunge, Job Ndugai amewataka Watanzania kuacha tabia kutothamini mafanikio au juhudi za watu mbalimbali wanazozionesha katika taifa hasa katika sekta ya biashara, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mgahawa wa Chakula katika Taarafa ya Pandambili Iliyopo njia Kuu ya Kutoka Dodoma Owenya Morogoro.
Ndugai ametoa kauli hiyo ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya aliyewahi kuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kudai kuwa kazi ya udereva bodaboda ni laana na ya kimasikini.
Amesema; "Kijana anza kufanya biashara halali, kazi ni kazi, achaneni na yule anayesema watu wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye, yule anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa, sasa ule si wenzawazimu tu."