Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji kutoa uamuzi pingamizi la kina Mdee leo

Mdee Mak.jpeg Jaji kutoa uamuzi pingamizi la kina Mdee leo

Fri, 2 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, leo Ijumaa, Septemba 2, 2022 inatarajia kutoa uamuzi wa pingamizi la Halima Mdee na wenzake kuhusiana na kiapo kinzani cha Chadema.

Uamuzi huo inatarajia kutolewa saa nane mchana na Jaji Jaji Cyprian Mkeha.

Kiapo hicho kinadaiwa kuwa na kasoro na miongoni kasoro hizo ni Chadema kukosea jina lao.

Agosti 26, 2022 Wakili wa waleta maombi (Halima Mdee na wenzake saba), Ipilinga Panya alieleza mahakama hiyo kiapo kinzani kilichowasilishwa na Chadema kimekosewa jina kwa makusudi ama kwa kutokukusudia.

Wakili Panya alidai jina lililowasilishwa kwenye kiapo kinzani ni bodi ya wadhamini inayosomeka Trustees of Chadema badala ya jina la bodi ya wadhamini inayosomeka Registerd Trustees of Chadema.

Panya aliieleza Mahakama hiyo kiapo kinzani hicho kimekosewa jina ama kwa makusudi au kukusudia kimeandikwa kwa jina ambalo wao wenyewe walilikataa kwenye maombi ya awali namba 16 ya mwaka 2022 yaliyotupiliwa mbali na Jaji John Mgeta

Wakili huyo amedai hoja hiyo ni hoja ya kisheria ambayo Mahakama inapaswa kuisikiliza kwanza kabla ya kuendelea na kusikiliza kwa shauri la msingi.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Mkeha iliahiridha kesi hadi leo, itakapoitwa kwa ajili ya kutoa uamuzi hukusiana kiapo hicho.

Mbali na Mdee, wabunge wengine ni Grace Tendega, Esther Matiko, Esther Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa na Nusrat Hanje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live