Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mutungi kuitisha kikao ili kujadili mvutano kati ya vyama na polisi nchini

Mutungi 660x400 Jaji Mutungi kuitisha kikao ili kujadili mvutano kati ya vyama na polisi nchini

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amesema anakusudia kuitisha kikao cha wadau, vyama vya siasa na jeshi la polisi ili kujadili mvutano uliopo kati ya jeshi la polisi na vyama vya siasa kuhusu mikutano na makongamano yanayoandaliwa na vyama hivyo.

“Tunafanya jitihada kuondosha mvutano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa, Msajili kama Mlezi wa Vyama vya Siasa niliwasiliana na IGP na tukakubaliana tuwaite Wadau, katika kikao hicho tutawaita Polisi wakiongozwa na IGP, Viongozi wa Vyama pamoja na Ofisi ya Msajili”——-Jaji Mutungi

“Lengo la kikao cha pamoja kati ya Polisi, Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama ni kukaa chini kuwa na maongezi kuhusiana na mikutano, makongamano n.k, nisingependa ifike mahala Watu waanze kuogopa, kila Mkutano wa Siasa Mapolisi wamejaa”———Jaji Mutungi

Kwa muda mrefu kumekuwa na sintofahamu kati ya jeshi la polisi na vyama vya siasa nchini hasa vyama vya upinzani ambapo kumeripotiwa matukio ya kukamatwa kwa wanachama wa vyama hivyo au kuzuiwa mikutano hata ya ndani kila wanapojaribu kufanya vikao.

Matukio hayo yamekua yakisababisha malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani wakidai kuwa chama tawala (CCM) kimekua kikifanya mkitano na vikao vyake bila bughudha ya jeshi la polisi hivyo kumtaka Rais Samia atoe kauli juu ya sauala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live