Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mutungi asema watasimamia sheria kuendesha vyama vya siasa

Jajipic Data Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema ofisi yake itajikita kufuata sheria katika uendeshaji wa vyama vya siasa nchini.

Jaji Mutungi ametoa kauli hiyo leo Desemba 15 wakati akifungua mkutano wa wadau wa vyama vya siasa nchini unaoendelea jijini Dodoma.

Mkutano huo umeitishwa na kugharamiwa na Serikali ambapo viongozi wa vyama vya siasa nchini, viongozi wa Serikali na Ofisi ya msajili wameshiriki huku mgeni rasmi akiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Sisi tunakomaa na sheria na tutasimamia sheria wakati wote lakini mikutano hii ikiwa ya mara kwa mara itasaidia watu kuwa na uelewa wa kutokukwenda kinyume na Sheria," amesema Jaji Mutungi.

Jaji amewapongeza vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu akimwambia Rais Samia kuwa kusalia Katika orodha ya vyama siyo kazi ndogo.

Amesema hatua wanazopitia siyo jambo la mchezo hivyo wote wanapaswa kupewa pongezi.

Advertisement Katika hatua nyingine Jaji amesema mchakato wa Kujenga jengo la Ofisi hiyo jijini Dodoma unaendelea vizuri.

Amesema jengo hilo ambalo litakuwa na ghorofa Saba, litajengwa na kutakuwa na kumbi za mikutano itakayojumuisha Ofisi ya uongozi wa Vyama vya siasa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz