Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mutungi aonya mchakato wa Katiba Mpya

Katibapic New Jaji Mutungi aonya mchakato wa Katiba Mpya

Wed, 10 May 2023 Chanzo: mwanachidigital

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameshauri kuwepo kwa muda wa kutosha katika mjadala wa Katiba Mpya ili kupata maoni toka makundi mbali mbali kabla ya kuitishwa kwa mkutano maalumu.

Akizungumza jana na runinga ya Azam, Jaji Mutungi amsema kuna watu wanatamani mkutano maalumu uitishwe kwa haraka, lakini serikali inaepuka hilo kwa sababu wajumbe wanaweza kuja na mawazo yao.

“Tukiitisha mkutano maalumu mapema tunaogopa wajumbe wanaweza kuja na mawazo yao badala ya uwakilishi wa makundi yao, sasa kwa muda uliotolewa kila mtu arudi kwenye kundi lake wajiandae na maoni kuntu ambayo wakija kuwasilisha yataleta sura nzuri ya Katiba,” amesema Msajili huyo.

Kuhusu wanasiasa Mutungi aliwataka kuheshimu kauli ya Wananchi na waone kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi wa kawaida kushiriki katika mchakato huo, ili kuleta taswira ya wote katika Katiba Mpya.

“Kauli yangu ninayotaka kuwapa wananchi, wanapaswa kuwa wavumilivu na kukubali mchakato unavyoendelea ili itusaidie kufika sehemu ambayo hatutakwama,”Jaji Mutungi amesema.

Hofu ya Msajili huyo wa Vyama vya Siasa nchini imejengeka kwa kile kilichowahi 2014 na hivyo kuwa kizingiti cha kukwamisha mchakato huo usiendelee, hivyo awaasa wanasiasa kuepuka hali hiyo isijitokeze tena baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuurejesha.

Mutungi ambaye ni mlezi wa Vyama vya Siasa nchini, alissisitiza chochote kinachopangwa kufanyika, umakini unapaswa kuzingatiwa kwa kurejea mapungufu yaliyofanya mchakato wa awali ukakwama.

Chanzo: mwanachidigital