Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mutungi akana kauli ya kusitisha mikutano ya Vyama vya Siasa

Mutungijaji Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amekana kauli ya baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti kuwa ametoa amri ya kusitisha mikutano ya ndani ya vyama vya siasa, na kuwa waliotoa taarifa hizo wamepotosha umma, iwe kwa makusudi ama kwa sababu zao binafsi.

Kupitia taarifa aliyoitoa leo Septemba 7, 2021, Jaji Mutungi amesema kuwa upotosaji huo ni kufuatia mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya jana Septemba 6 jijini Dar es Salaam kuhusu adhma yake ya kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro pamoja na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ili kutafuta suluhu ya mivutano iliyojitokeza baina ya Jeshi la Polisi na vyama vya siasa hususani vinavyotaka kufanya makongamano na mikutano ya ndani.

Amesisistiza kuwa, hajatoa zuio la mikutano lakini kwa busara ya kawaida aliomba, wakati jitihada hizo zinaendelea, vyama vijizuie kwa muda kuendelea na shughuli zinazosababisha kutokea kwa mivutano hiyo.

Kwa zaidi ya miaka 6, kumekuwepo na sintofahamu kuhusu uhuru wa kisiasa nchini, na mara kadhaa Rais Samia amenukuliwa akisisitiza kuhusu nia yake ya kukutana na Vyama vya Upinzani nchini kujadili tofauti zilizopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live