Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mutungi: Vyama havijawahi kulalamika kuzuiwa mikutano

66196 Pic+mutungi

Wed, 10 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema ofisi yake haijawahi kupokea malalamiko ya maandishi kutoka vyama vya upinzani kuhusu kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

Kauli ya Jaji Mutungi imethibitishwa na katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ambaye amesema chama chake hakijawahi kufanya hivyo, akiamini hilo lipo juu ya uwezo wake.

Jaji Mutungi alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu malalamiko yanayotolewa na vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano hiyo huku CCM ikiruhusiwa.

Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally juzi alianza ziara ya siku nne mkoani Kilimanjaro, mikutano inayofanana na ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani lakini wamekuwa wakizuiwa.

Mara kadhaa, viongozi wa upinzani wamekuwa wakilalamikia jambo hilo katika maeneo mbalimbali na katika Bunge la bajeti lililomalizika Juni 28, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kwa nyakati tofauti walihoji kuhusu suala hilo.

Alisema vyama hivyo vinapaswa kutuma malalamiko yao kwa maandishi ili ofisi yake ipate cha kuanzia? “sasa wao wenyewe hawalalamiki lakini nyie waandishi mnalalamika, huoni kama wanaweza wakawaruka.”

Pia Soma

Mwaka 2016, Rais John Magufuli alitoa tamko la kuzuia mikutano ya hadhara na Januari 23 mwaka huu alifafanua akisema hakuna kiongozi aliyezuiwa kufanya mkutano katika jimbo lake, bali kilichozuiwa ni kwenda kufanya mikutano katika majimbo ya wengine tena kwa fujo.

Viongozi kadhaa wakiwamo wa Chadema, ACT Wazalendo, baadhi ya wachambuzi wa duru za kisiasa nchini wamesema Jeshi la Polisi linahusika katika zuio hilo kwa kusimamia utoaji wa vibali ambao walisema hauna uwianosawa kwa vyama vya siasa.

Tangu Julai 6, Dk Bashiru amekuwa akifanya mikutano mbalimbali ikiwamo kushiriki uzinduzi wa Boma la Eunoto katika Kijiji cha Mti Mmoja wilayani Monduli, pamoja na vikao vya ndani viwili vilivyofanyika katika Wilaya ya Siha, Kilimanjaro.

Katika kikao kilichofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba juzi, Dk Bashiru alisema ameanza ziara hiyo katika Mkoa wa Kilimanjaro kimkakati, akisema mkoa huo na Jimbo la Hai si ngome ya Chadema.

Februari mwaka huu, Zitto akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama, alizuiliwa na kutakiwa kuripoti kituo cha Polisi Mgeta, Mvomero, Morogoro kwa mahojiano.

Katika kipindi hichohicho, Dk Bashiru alifanya mikutano kadhaa mkoani Morogoro na katibu wa itikadi na uenezi CCM, Humphrey Polepole alifanya ziara Arusha.

Hukohuko, Morogoro, Polisi walisitisha mkutano wa hadhara wa Chadema uliokuwa umepangwa kufanyika Juni 16 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege.

Jana, akizungumzia kauli ya Jaji Mutungi kuhusu mikutano hiyo, Dk Mashinji alisema, “malalamiko ya mikutano ya hadhara hatujapeleka. Tunajua hana ubavu wa kuifanyia chochote kwa sababu aliyeagiza ni bosi wake.

Alipoulizwa pengine hatua ya kutopeleka malalamiko hayo inaweza kuwa sababu ya msajili huyo kujenga hoja ya kutoshughulika na malalamiko hayo, Dk Mashinji alisema, “hawezi bana asidanganye watu.”

Pamoja na uamuzi huo, Dk Mashinji alisema kuna malalamiko mengi yanayohusu malezi ya ofisi hiyo ambayo walishampelekea lakini hayafanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe alisema kauli ya Dk Bashiru ni utetezi unaoonyesha wazi kuwa Serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake.

Alisema kiongozi huyo ametoa kauli hiyo akijua kwamba wananchi hawana la kufanya.

Alisema, “mambo haya yawafanye wananchi watambue kuwa hawa watu ni wababaishaji. Miaka yote miradi inafanywa na fedha gani halafu leo utoe ahadi ushindwe kutekeleza kwa kisingizio cha miradi?”

Chanzo: mwananchi.co.tz